Kwa kinachoendelea hapa viongozi wa Yanga wamesema njia ya kupata ushindi inaonekana na sapoti ni kubwa huku mashabiki wengi kwenye mitandao ya Yanga wakitaka Clement Mzize na Fiston Mayele waanze katika kikosi cha leo.
Kundi kubwa la Watanzania lilijitokeza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo kuipokea na kuilaki Yanga huku baadhi wakiwa wamevaa jezi za timu hiyo, wengine wakivaa za Simba na wapo waliovaa jezi zilizoandikwa Tanzania.
Mfano mwingine wa hilo ni Mtanzania, Swalehe Madjapa ambaye amesafiri kutoka Tanzania hadi Afrika Kusini kuisapoti Yanga huku akiwa ni mwanachama na shabiki wa Simba.
VIGOGO KIBAO, WATAMBA
Msafara wa Yanga Afrika
Kusini umehusisha kundi kubwa la viongozi wa serikali na wadau wa timu
hiyo hasa wale wenye uwezo wa kifedha kwa lengo linaloonekana kwenda
kuipa hamaa timu hiyo ili iweze kutinga hatua ya fainali ya mashindano
hayo.
UWANJA WA YANGA MTEGO
Mechi
hiyo imepangwa kuchezwa katika Uwanja wa Royal Bafokeng ambao Marumo
imeutumia kwa mechi zake mbili kati ya tano zilizopita za Kombe la
Shirikisho Afrika.
Yanga inapaswa kufanya kazi ya ziada kumaliza
ubabe wa Marumo Gallants kwenye Uwanja huo kwani timu hiyo ya Afrika
Kusini, imeshinda mechi zake zote mbili ilizocheza uwanjani hapo dhidi
ya Al Ahli Tripoli na Pyramids FC, imeshinda zote bila kuruhusu bao na
imepachika mabao manne.
Kimsingi Marumo Gallants sio timu rahisi
inapokuwa nyumbani kwa vile katika mechi zote tano za mashindano hayo
ilizocheza nyumbani, imeshinda zote, imefunga mabao 13 na kuruhusu nyavu
zakekutikiswa mara tatu.
Royal Bafokeng ni miongoni mwa viwanja 10 vilivyotumika katika fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika Afrika Kusini mwaka 2010 ambapo uliandaa idadi ya mechi sita, tano zikiwa za hatua ya makundi na moja ikiwa ni ya raundi ya 16 bora.
Ni uwanja wa nyasi za kawaida uliofunguliwa rasmi mwaka 1999 na
kufanyiwa marekebisho mwaka 2009 huku ukiwa unaingiza idadi ya mashabiki
44,530.
Suala la chakula halionekani kama ni changamoto kwa Yanga
hapa Afrika Kusini kwani vyakula vingi vilivyozoeleka nyumbani Tanzania,
vinapatikana hapa.
Ulipotua Johannesburg, ulipokelewa na Balozi wa Tanzania nchini humo,
Meja Jenerali Gaudence Milanzi pamoja na maofisa wa ubalozi kutokea
Pretoria ambako upo.
Kutoka nyumbani, upande wa serikali unaongozwa
na Naibu Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo, Hamis Mwinjuma lakini
pia kwa upande wa Yanga, mdhamini na mfadhili wa timu hiyo, Bilionea
Ghalib Said Mohammed (GSM) ni miongoni ataongoza kundi la vigogo wa timu
hiyo waliopo hapa.
Yanga mjini Rutenburg wamefikia katika hoteli ya
Royal Marang ambayo gharama ya chini ya chumba kimoja ni Randi 2140 (Sh
264,900).
Hoteli hiyo mbali ya kuwa na kumbi ya gym ya kisasa kwa ajili ya
mazoezi, ina mabwawa ya kifahari ya kuogelea, viwanja vya kisasa vya
michezo ya mpira wa wavu na tenisi lakini pia ina kumbi za michezo ya
kompyuta.
Kuna kumbi tano kubwa na za kifahari za mikutano katika
hoteli hiyo iliyopo jijini Rusternburg. Kwa kukaa katika hoteli hiyo
tangu jumapili hadi siku ya mchezo, Yanga itakuwa imetumia zaidi ya Sh
100 milioni kwa gharama za malazi, chakula na nyinginezo.
Rusternburg
ambako hoteli hiyo ya Royal Marang ipo, lipo Kaskazini Magharibi mwa
jiji maarufu la Afrika Kusini la Johannesburg na makao makuu ya nchi
hiyo, Pretoria.
Post a Comment