NGUMI NA MAISHA: MIKE TYSON NA HADITHI YA KUVUTIA

Na Emmanuel Masuza

Mike Tyson alizaliwa na kukulia katika mazingira magumu huko Brooklyn New York City nchini Marekani, Alikulia katika hali ngumu ya maisha akiwa na mama yake Lorna Smith Tyson Baba yake hakuwepo sana katika maisha yake, Alijikuta akijihusisha naq makundi ya uhalifu akiwa bado mdogo, na hadi kufikia umri wa miaka 13 tayari alikuwa amekamatwa mara 38 kwa makosa tofauti ya uhalifu.

Alipoanza shule Michel Tyson aligunduliwa na kocha wa ndondi Bobby Stewart ambaye aliona kipaji chake cha ndondi na kumtambulisha kwa Cus D’Amato kocha maarufu wa ndondi. D’Amato aliamua kumlea na kumfundisha Mna hata kuwa mlezi wake rasmi baada ya kifo cha mama yake mwaka 1982

Mike Tyson alianza ndondi za kulipwa mnamo 1985 akiwa na umri wa miaka 18 Alianza kwa kishindo akishinda mapambano yake mengi kwa KO (Knockout). Kati ya mapambano yake 15 ya kwanza yote alishinda kwa KO jambo lililomfanya kuwa gumzo katika ulimwengu wa ndondi.


Mnamo Novemba 22, 1986, akiwa na umri wa miaka 20 alimpiga Trevor Berbick na kuwa bingwa wa uzani wa juu wa WBC akivunja rekodi ya kuwa bingwa mwenye umri mdogo zaidi katika historia ya ndondi za uzani wa juu.

Mwaka 1987, alitwaa mataji ya WBA na IBF kwa kuwashinda James Smith na Tony Tucker, hivyo kuwa bingwa wa kwanza wa uzani wa juu kushikilia mataji yote matatu kwa wakati mmoja.

Baada ya kufanikiwa kwa muda mfupi maisha ya Mike Tyson yalianza kuporomoka Mnamo 1990, alishindwa kwa KO na James “Buster” Douglas katika pambano lililotikisa ulimwengu wa ndondi, kwani Douglas hakuwa anapewa nafasi ya kushinda.

Mwaka 1992, Tyson alihukumiwa kifungo cha miaka 6 jela kwa kosa la ubakaji, lakini aliachiliwa baada ya kutumikia miaka mitatu.

Baada ya kutoka gerezani alirudi ulingoni na kushinda mataji ya WBA na WBC lakini mwaka 1997 alihusika katika tukio maarufu la kung’ata sikio la Evander Holyfield lililosababisha apokonywe leseni ya ndondi kwa muda.


Tyson alistaafu rasmi ndondi mwaka 2005 baada ya kupoteza pambano lake dhidi ya Kevin McBride. Baada ya kustaafu, alijihusisha na biashara, uigizaji, na hata kuandika kitabu cha maisha yake kiitwacho Undisputed Truth

Amekuwa pia akijihusisha na masuala ya uhamasishaji wa afya ya akili na biashara ya bangi kupitia kampuni yake ya Tyson Ranch

Mike Tyson anahesabiwa kama mmoja wa mabondia bora wa uzani wa juu kuwahi kutokea. Pamoja na changamoto za maisha yake, bado anaheshimiwa kwa kasi yake, nguvu zake, na ushawishi wake katika mchezo wa ndondi

Leo hii, Tyson anaendelea kuwa mtu mashuhuri akishiriki mahojian vipindi vya televisheni



0718431472

Emmasolomon825@gmail.com


0/Post a Comment/Comments