STARS USO KWA USO NA MOROCCO

 

Na Emmanuel Masuza

Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, inatarajiwa kushuka dimbani leo saa 6:30 kwa saa za Afrika Mashariki kumenyana na Morocco katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026.

Mechi hii ni sehemu ya kampeni za kufuzu kwa michuano hiyo mikubwa ya soka duniani, na Taifa Stars inapigania kupata matokeo mazuri dhidi ya moja ya timu bora barani Afrika.

Hadi sasa, Morocco inaongoza Kundi E akiwa na alama zake 12 huku Taifa Stars ikishika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi hilo ikiwa na alama 6. Ushindi katika mechi ya leo utakuwa muhimu kwa Tanzania kuimarisha nafasi yake katika mbio za kufuzu. Pamoja na kwamba Morocco ni timu yenye uzoefu mkubwa wa kimataifa, Taifa Stars inatarajia kupata matokeo mazuri kwa kutumia ari ya hali ya juu na ari ya wachezaji wake.

Mechi hii inatarajiwa kuwa na ushindani mkali, huku mashabiki wa soka wakisubiri kuona iwapo Taifa Stars inaweza kuibuka na ushindi dhidi ya wababe hao wa soka barani Afrika.


0718431472

Emmasolomon825@gmail.com


0/Post a Comment/Comments